this is the fantastic blog on sharing and discussing the word of GOD welcome and enjoy been here contact: uscfamucta@gmail.com
Saturday, August 13, 2011
Tuzidi kumshika Mungu tunapokuwa TP
Wapendwa katika bwana, Bwana Yesu asifiwe. Najua kwa kipindi hiki upo katika mazingira Tp, ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kutuweka hai mpaka leo. Ni wengi waliotarajia kufika leo lakini wameshindwa. Sasa tunapenda kuwakumbusha kuwa Mungu wetu anaishi na anaweza, hivyo tumtumaini yeye atatupigania daima. Magumu yote utakayokutana nayo huko, mwombe Mungu ashughulike nayo, maana yanaweza kuwa mazito zaidi kwako. Mungu awabariki na Tp njema
Tuesday, June 28, 2011
Wachungaji Msitangazie washirika dhambi ya mtu mwingine!
“Mchungaji unapotangaza dhambi/makosa ya mtu kwa washirika/waumini kinachotokea ni kwamba yule mtu hata kama ameshatubu kwa Mungu wale washirika watabakia wakimhukumu “fulani alitenda dhambi hii”. Kwa kufanya hivyo watu hao wanabakia na dhambi hiyo hadi siku yao ya kufa. Maana mtu akitubu Mungu humsamehe lakini watu ni vigumu sana kusahau.
Na wewe mtu uliyeokoka, mtu akitenda dhambi achana naye, usiweke dhambi yake moyoni mwako bali songa mbele katika kumwangalia Yesu”
Mwinjilisti Obadia alipokuwa akihubiri katika mkutano wa Injili mjini Arusha tarehe 22, June, 2011.
Friday, June 24, 2011
KWA NINI IMANI YA MWANAMKE MKANANAYO ILIONEKANA KWA KUBWA?
Na: Patrick Sanga
Nakusalimu kwa jina la Bwana, amani na iwe kwako.Katika Mathayo 15:21-28 maandiko yanasema “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yaka tangu saa ile”
Katika zamu hii nimeona vema kujibu swali jingine linalohusu imani ya mwanamke Mkakanayo. Huyu Mama alikuwa mwenyeji wa nchi ya Kanaani ambayo ilikuwa karibu na pwani ya Bahari ya kati kutoka Sidoni. Kwa bahati nzuri Yesu alikuwa amekwenda katika miji ya Tiro na Sidoni kihuduma, ndipo akakutana na mama huyu ambaye alikuwa anahitaji msaada wa Yesu apate kumponya bintiye.
Haikuwa jambo rahisi kwa Yesu kuachilia uponyaji uende kwa yule binti. Lakini baada ya mvutano wa muda mrefu, Yesu alimwambia yule mama ‘Imani yako ni kubwa, na iwe kwako kama utakavyo’. Sasa swali la msingi ninalotaka kujibu ili nasi tupate kujifunza ni hili; kwa nini imani ya yule mama ilionekana kuwa kubwa kiasi cha kuamua uponyaji utoke kwa Yesu na kwenda kwa binti yake na kumponya saa ile ile?
Yafuatayo ni mambo matatu yaliyompelekea Yesu kusema, Mama, imani yako ni kubwa;
- Kutokukata tamaa/kuchoka.
- Aliyapuuza/hakujali maneno ya wanafunzi na wale walifuatana na Yesu.
- Alikuwa na ufahamu wa masuala ya kiroho(imani).
Ile kuendelea kuomba kwa unyenyekevu kwa Bwana amponye bintiye na pia kujibu kwamba hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao, ilidhihirisha kwamba ni lazima huyu mama, ingawa alikuwa Mkaanani kuna namna alikuwa ana ufahamu wa mambo ya imani katika Kristo (neno la Mungu). Kwa hiyo hakikumsumbua watu (Yesu) wanasema nini, ndani yake alikuwa na ufahamu na imani kwamba hakuna jambo la kumshinda Bwana, na hivyo ndani yake akazidisha uhakika kwamba bintiye atapona tu.
Naam ile kusema hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao, kauli hili ilimfanya Yesu kuachilia uponyaji kwenda kwa binti yake saa ile ile na ndipo akasema, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo.
Sijui kama umeliona jambo hili mpenzi msomaji, imani ya yule mama ili kuwa kubwa kiasi cha kutenda kwa kadri ya matakwa yake kuhusu binti yake. Ni imani iliyoje kutoka kwa mwanamke wa pande za Kaanani, mahali ambako kwa mujibu wa Yesu hapakuwa kipaumbele chake kuwafikia/kuwasaidia. Naam imani ya huyu mama ilivuka fikra na mipaka hiyo na kumfanya Yesu kuachilia uponyaji kawa kdari ya matakwa na muda anaotaka yule mama (Such a wonderful faith).
Tunajifunza nini?
Naam hata leo kuna sababu kubwa tatu zinazofanya watu washindwe kupokea majibu ya mahitaji yao au yale wanayoamini kwamba Mungu atawafanyia;
- Kukata tamaa
- Maneno ya kusikia
- Kukosa ufahamu wa neno la Mungu kuhusu imani
Kwa sababu imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, tena bayana ya yale yasiyoonekana (Waebrania 11:1), tunaweza kusema kwamba ukubwa wa imani ya huyu Mama ulitokana na uhakika aliokuwa nao kwamba Yesu atamponya mwanawe licha ya upinzani aliokutana nao kuhusu imani yake. Si tu kwamba yule mama alikuwa ana amini Yesu atamponya bintiye, bali yeye alishaona kwa imani kwamba Yesu amemponya mwanawe na hivyo alikuwa anang’ang’ania utimilifu wa kile alichoona kwa imani. Naam alikiona alichokiamini, hivyo alikijua anachokiamini, akakipata alichokiona.
Naam hakikisha unaongeza imani yako kila siku, ili ifikie na kuzidi ile ya Mwanamke Mkananayo na hivyo iweze kuamua majibu kwa kadri ya matakwa na muda wako kutoka kwa Yesu.
Mungu akubariki.
Wednesday, June 22, 2011
wana -USCF waaswa kuhudhuria kanisani
wana- ukwata wa hapa SAUT TABORA wametakiwa kuhudhuria kanisani ili kushiriki ibaada ya pamoja na wan USCF wenzao katika ibaada za kila siku za jumapili ambazo hufanyika kila jumapili kuanzia saa 2-4 asubuhi.
akiongea na blog hii mwenyekiti na katibu wa uscf kwa nyakati tofauti walisema yakuwa kuwa katika kipindi hiki cha chuo kikuu si kigezo cha kuacha kuhudhuria ibaadani na kutomwabudu Mungu aliyempa uhai na uwezo wa kutembea. hivyo basi kila mwana ukwata wanapaswa kuhudhuria ibaada hizi muhimu katika kukua kiroho
akiongea na blog hii mwenyekiti na katibu wa uscf kwa nyakati tofauti walisema yakuwa kuwa katika kipindi hiki cha chuo kikuu si kigezo cha kuacha kuhudhuria ibaadani na kutomwabudu Mungu aliyempa uhai na uwezo wa kutembea. hivyo basi kila mwana ukwata wanapaswa kuhudhuria ibaada hizi muhimu katika kukua kiroho
Monday, June 20, 2011
USCF AMUCTA Wateua kamati mbalimbali
viongozi wa USCF hapa SAUT TABORA wameteua kamati mbalimbali za kuweza kufanikisha kazi za uscf kusonga. kamati hizo ziliteuliwa wakati wa kikao cha kamati kuu cha USCF kilichofanyika jumapili iliyopita ya tarehe 19/6/2011. kikao hicho kikiwa na wajumbe kadhaa ambao ni
KIULA OSWALD-MWENYEKITI
REGINA PHAUSTINE-M/KITI MSAIDIZI
MESHACK JACKSON- KATIBU
SUBIRA MANASE- M/KATIBU
SINEDA KADASO-MHAZINI
JASTIN JOHN-MWAKILISHI
katika kikao hicho kiliteua kamti zifuatazo na viongozi wake
KAMATI YA UINJILISTI
1.SIJALI MGONDE-MWENYEKITI
2.RAFAEL PETRO-KATIBU
KAMATI YA UKARIMU
1.DAMARIS KASIGA-MWENYEKITI
2.PETER SIMONI-KATIBU WAKE
mwenyezi MUNGU na aubariki uteuzi huu
Subscribe to:
Posts (Atom)